Monday, January 30, 2012


MECHI KATI YA WATANGAZAJI WA RADIO NA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI LAFANA KATIKA VIWANJA VYA TTCL- KIJITONYAMA.
Siku iliyokuwa inasubiriwa na Watanzania kuhusiana na mechi kali kati ya Watangazaji, mapromota na waimbaji wa nyimbo za injili waliotegemea kupambana na wacheza filamu (Bongo Movie). Zoezi hili halikuweza kufanikiwa kutokana timu ya Bongo Movie kuwa na mualiko Zanzibar katika tamasha lao la ZIFF. Badala yake kamati iliamua kupambanisha kati ya Waimbaji wa nyimbo za injili na Watangazaji wa radio za kikriso Tanzania.



Tamasha lilionekana kuvutiwa na Watanzania wengi. Timu ya Watangazaji ilipigwa bao 2 na Waimbaji kuibuka washindi kwa mabao 5. Mfungaji bora wa watangazaji alikuwa Mtangazaji wa Channel Ten ambaye alikuwa mtangazaji wa radio ya Praise Power, Boniface Magupa aliyefunga mabao mawili na kujipatia Tsh. 5000 kama mfungaji bora.

Mbali na mashindano ya mpira ya miguu kulikuwa na mchezo wa kufukuza kuku ambapo Mwimbaji wa Glorious Celebration, Jessica Honore alijishindia kuku na upande wa watangazaji wa radio, Yusuf Magupa wa Praise Power alishinda na kujipatia kitoeo cha kuku.

Waimbaji kama Martha Mwaipaja, Martha Ramadhan, Glorious Celebration na wengine wengi walionekana kugusa mioyo ya watu kwa nyimbo zao zenye kumwinua Mungu wetu.
 Baadhi wa wachezaji wakiwa katika kiwanja cha shule ya Kenton Sinza wakijiandaa kuelekea katika uwanja wa Posta-Kijitonyama.
Stori zikiendelea.....

No comments:

Post a Comment